Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Darul Qur'an, "Kauthar al-Nabi" ilifunguliwa takriban miezi 6 iliyopita kwa ajili ya kutoa Sayansi (Elimu) ya Kidini kwa Watoto na Vijana wa Kishia katika Mji wa "Gorshak" huko "Helmand" Jimbo la Kusini mwa Afghanistan. Takriban Wanafunzi 200 wa Qur'an wa Kiume na wa Kike wanajishughulisha na Sayansi (Elimu) ya Kidini katika "Darul Qur'an" hii, ambayo inafanya kazi kwa msaada wa Wakubwa - (Wazee) - wa Kishia wa jimbo la Helmand.
19 Septemba 2024 - 11:10
Msimbo wa Habari: 1486542